MARUFUKU TANESCO KUKATA UMEME BILA SABABU MAALUM
Naibu waziri wa nishati mh Subira
Mgalu amewagiza watendaji wa wa Tanesco kuhakikisha kuwa hawakati umeme bila sababu maalum ili
kuwaondolea wananchi adha ya kukosa nishati hiyo
Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua mitambo ya umeme katika kituo cha kipawa jijini Dar es salaaam na mradi wa
TEDAP unaoshughulikia upanuzi na ujenzi
wa vituo vya kupozea umeme.
Amesisitiza kuwa umeme ukatike pale inapositahili na endapo tatizo
limetokea kwenye mifumo ya umeme ni vyema kutoa taarifa mapema kwa wananchi.
No comments