USAID YAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI
Mkurugenzi mkazi wa shirika la misaada ya kimataifa la
marekani USAID bwana Andy Karas amepongeza jitihada za serikali ya tanzania
kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF katika kuwafikia wananchi
wanaokabiliwa na umaskini kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini ambao umeanza
kuonyesha mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Bwana Karas ameyasema hayo wakati alipokutana na walengwa
wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli
katika halimashauri ya wilaya ya Iringa ambako licha ya kuelezwa namna TASAF
inavyoendelea kutekeleza mpango huo lakini pia ameshuhudia namna walengwa wa
mfuko huo walivyoboresha maisha yao kwa kutumia fedha za ruzuku za mfuko huo.
Amesema kuwa hamasa inayoonyeshwa na walengwa wa mpango
wa kunusuru kaya masikini katika kujiletea maendeleo kwa kuanzisha miradi
midogomidogo kwa kutumia fedha zinzotolewa na serikilali kupitia tasaf
imelivutia shirika hilo na kuahidi kuwa litaendelea kushirikiana na serikali ya
tanzania katika kuboresha utaratibu wa kuwainua wananchi kiuchumi.
Hata hivyo bwana karas amesema utaratibu wa kuwafikia na
kuwasaidia moja kwa moja wananchi wanaoishi katika mazingira magumu ya kiuchumi
umekuwa ukitumika katika nchi nyingi duniani na umeonyesha mafanikio makubwa
kwa kusimamia shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kaya maskini.
No comments