WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII ATOA AGIZO
Katibu mkuu wa wizara ya mali asili na utalii mh. Gaudence Milanzi amesema
agizo la waziri wa mali asili na utalii Mh Hamis Kigwangalla kuhusu kusimamishwa kazi mkurugenzi wa
wanyama poli profesa Alexander Songorwa
litatekelezwa baada ya utaratibu kufuatwa.
Dk Kigwangallah aliagiza profesa Songorwa kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma
kadhaa baada ya kufanya ziara katika
hifadhi ya taifa ya serengeti ambapo aliieleza taasisi ya kuzuia na kupambana
na rushwa Takukuru kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo na hatua sitahiki
zichukuliwe.
Hata hivyo mwaka 2014 mkurugenzi huyo alisimamishwa kazi na aliyekuwa
waziri wa wizara hiyo Lazaro Nyalandu kutokana na kutajwa katika operesheni
tokomeza na kamati ya bunge ya ardhi, maliasili na utalii ambapo baadae
alirejeshwa kazini.
No comments