MRUDISHIE MWENYE HAKI ,HAKI YAKE UEPUKE ADHABU YA MUNGU
Watu wengi wameifunga milango ya baraka wao wenyewe bila kujua na
wamejikuta wakiwa kwenye mateso makubwa na wanapo itafuta suluhu ya mateso
hayo hawaipati jambo linalowafanya
wayaone maisha yao kama ni ya bahati mbaya hapa duniani.
Kuna jambo moja tu napenda kukumbusha wakati mwingine unaweza kuwa
unalifahamu lakini hauli elewi kwa kina,kitu kinachoweza kuyaua au kuyangamiza
maisha yako kwa haraka ni DHURUMA,kuchukua na kumiliki kitu, haki,mali ya mtu
kwa nguvu ,yaani bila ridhaa yake.
Wapo watu wengi ambao maisha yao yameharibika na wakati mwingine mwisho wa
maisha yao umebaki kuwa historia katika uso wa dunia na husimliwa na kila mtu
kwa sababu ya dhuruma walizozifanya wakati wa uhai wao.
Ukisoma Biblia katika kitabu cha Mwanzo 20:13-18 ,utaziona habari za
Abimeleki,aliyekuwa mfalme wa Gerari.Abimeleki,mkewe na wajakazi wake
walifungwa matumbo wasizae kwa sababu Abimeleki alimchukua Sara kwa nguvu mke
wa Ibahimu.
Na hii inadhihirisha wazi kuwa dhuruma ni jambo baya sana katika
maisha.Dhuruma inaweza kufunga kila mlango wa mafanikio katika maisha ya mtu,
unaweza kuwa mfanyabiashara mzuri lakini mara tu baada ya kufanya dhuruma
utaona biashara yako inaanza kunyauka na mwishowe unaishiwa kabisa.
Wapo watu wengi toka waingie kwenye ndoa ni miaka mingi imepita lakini
hawajapata mtoto na mara kadhaa wamefanya vipimo na taarifa zinaonyesha hawana
tatizo lolote la kiafya linalowafanya wakose mtoto hili si jambo la kushangaza
kwani tunaona Abimeleki na mkewe pamoja na watu wa ndani mwake wanafungwa
matumbo wasizae kwa sababu ya dhuruma, aliyoifanya Abimeleki. Usishangae kuona
wanao wakifeli mitihani pamoja na gharama nyingi unazozitumia ikiwa ni pamoja
na kuwapatia masomo ya ziada, unajitahidi kuwatunza vizuri lakini wanakuwa watu
wasiokuwa na mbele wala nyuma katika maisha yao kumbe kuna mahali umekosea.
Ukisoma Mwanzo20:7 utaona Mungu mwenyewe anamwambia Abimeleki,asipomrudisha
mke wa Ibrahimu atakufa yeye na watu wote alionao
Hivyo dhuruma inapelekea kifo kama hautakuwa tayari kurudisha haki ya mtu
au watu uliowadhurumu.
No comments