Heade

WANAFUNZI SITA (6) WAFARIKI DUNIA KWA MLIPUKO WA BOMU KAGERA

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi 6 kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa kwa bomu ni kutokana na mwanafunzi kuokota bomu hilo akidhani ni chuma chakavu akitarajia kwenda kukiuza
Amesema kumekuwa na tabia ya kuuza vyuma chakavu katika kijiji hicho ambapo mnunuzi huwapatia wanafunzi hao madaftatari.

Kwa upande wa kamanda wa kikosi cha kulinda mipaka cha jeshi la wananchi Tanzania JWTZ wilayani Ngara meja TR Mutaguzwa amesema bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa lingeleta athari zaidi.

No comments

Powered by Blogger.