MUGABE AONEKANA HADHARANI
Rais wa Zimbabwe Robart Mugabe leo ameonekana kwa mara ya kwanza tangu
jeshi la nchi hiyo lichukue udhibiti wa nchi ikiwemo kituo cha Runinga cha
Taifa nchini humo toka siku ya jumatano.
Bwana Mugabe amekua chini ya kizuizi cha nyumbani kwa siku kadhaa huku
kukiwa na mvutano wa nani atakae mrithi.
Jeshi la Zimbabwe limesema lilikua kwenye mazungumzo na Mugabe na
litaujulisha umma matokeo ya mazungumzo hayo.
Rais huyo aliyedumu madarakani kwa muda mrefu na mwenye umri mkubwa Duniani
alianza kuiongoza Zimbabwe tangu mwaka 1980.
No comments