SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI ENDELEVU KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO NJITI
.
Mkurugenzi wa huduma za kinga katika wizara ya afya, Maendeleo ya jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto,Dkt. Neema Rusibamayala. Amesema serikali imeweka
mikakati endelevu ya kupunguza vifo vya watoto njiti kwa kushirikiana na wadau
wa sekta ya afya nchini.
Amesema hayo leo katika hospitali ya taifa Muhimbili (MNH), alipokua katika
maadhimisho ya mtoto njiti duniani ambayo huadhimishwa novemba17 kila mwaka.
Pia mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya taifa Muhimbili(HNM)profesa
Lawrence Museru amesema kua hospitali hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
inaendelea kutoa mafunzo ya mda mfupi na mrefu kwa wauguzi na madaktari wa
kitengo cha watoto wachanga ili kuongeza ufanisi wa kazi.
No comments