RAILA ODINGA AREJEA NCHINI KENYA
Umati mkubwa wa wafuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Nasa umejitokeza kumpokea kiongozi wao
Raila Odinga katika sherehe zilizogeuka kuwa za vurugu,mabomu ya machozi na
mapambano ya kukimbizana na polisi.
watu wawili wanadaiwa kufariki dunia baada na kinachosadikika kuwa ni
risasi wakati polisi wakiwatawanya watu waliokua wanatembea kutoka uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).
Licha ya ulinzi uliokuwepo na moshi wa mabomu ya machozi wafuasi wa Nasa
wapatao 200 wakiwemo wanawake walifanikisha kupita utepe uliowekwa na vyombo
vya usalama na kuingia hadi ndani ya uwanja.
No comments