MUGABE MIAKA 37 SI HABA
Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia
kuondoka kwa rais Robert Mugabe
madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa wake.
Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano
-ataapishwa mjini Harare. nchini
zimbabwe.
Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi
kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang'atuke .
Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza
"utamaduni wa ufisadi".
Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku
ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe
No comments