WANNE WAUWAWA KWA SHAMBULIZI LA KUJITOA MHANGA AFGHANISTAN
Raia wanane wameuawa hii leo katika shambulizi la kujitoa muhanga
lililofanyika katika jimbo la Nangarhar mashariki mwa Afghanistan.
shirika la habari la dpa nchini humo
limesema kuwa watoto wawili ni
miongoni mwa waliouawa . Shambulizi hilo limefanyika mbele
ya nyumba ya kamanda wa zamani wa kikosi maalumu cha ulinzi nchini Afghanistan,
ALP wanasadikiwa kuhusika
katika tukio , mji wa Jalalabad,
ambao ni mji mkuu wa jimbo la Nangarhar. ALP ni kundi la wanamgambo wanaolipwa
na waliopewa mafunzo na serikali ya Afghanistan kwa kushirikiana na Marekani
ili kuweka ulinzi dhidi ya mashambulizi ya waasi wa Taliban katika vijiji na
wilaya nchini humo.
Hadi sasa hakuna kundi lililodai
kuhusika na shambulizi hilo, ingawa katika kipindi cha miezi kadhaa kundi la
Taliban limekuwa likijihusisha na mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama na
watumishi wa serikali.
No comments