MWANA CHUO MMOJA AJINYONGA TABORA
Mwanachuo mmoja wa chuo cha utumishi
wa umma tawi la Tabora anayefahamika kwa jina la Raphael Kadesha (22) amefariki
dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tai ya kuvaa shingoni.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora
Graifton Mushi amesema tukio hilo limetokea jana asubuhi ambapo marehemu
alifunga tai juu ya kitanda chake.
Amesema marehemu alikua mwanafunzi wa kozi ya Utawala ngazi ya cheti katika
chuo hicho na kusema chanzo cha kifo chake bado
hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi.
Naye mkurugenzi wa chuo hicho Dk Ramadhani Marijani amewataka wanachuo kuwa
watulivu wakati jeshi la polisi kuendelea na uchunguzi.
No comments