WATU 106 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UHALIFU KATIKA KITUO CHA MABASI UBUNGO
Jeshi la polisi kanda maalum jijini Dar es salaam limewakamata watu 106 kwenye kituo cha mabasi ya mikoa Ubongo kwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi.
Kamanda wa polisi kanda maalum jijini Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema kati ya watuhumiwa 106 waliokamatwa katika oparesheni iliyofanyika katika kituo hicho watuhumiwa 95 walikutwa na makosa ya kubughudhi abiria, kuibia abiria ,kuuza tiketi bandia na kujivisha sare za mawakala wa mabasi huku wakijua kwamba si wahusika.
Amesema watuhumiwa wengine 11 baada ya uchambuzi wamebainika kuwa na kesi mbalimbali zinazoendelea na wamepelekwa kituo kikuu cha magomeni kuendelea na tuhuma zinazo wakabili.
Aidha kamanda Mambosasa amesema msako huo utakuwa endelevu katika stendi za mbezi , temeke na vituo vyote vya mabasi ya abiria na mizigo.
No comments