RAIS WA KENYA UHURU KENYATA ATARAJIWA KUAPISHWA
Rais wa kenya mhe, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa
kuwa rais kwa muhura wa pili baada ya mahakama ya juu kufutilia mbali kesi
ambazo zilikuwa zinapinga ushindi wake katika uchaguzi wa marudio uliofanyika
tarehe 26 october mwaka huu.
Aidha kifungu cha 141 (1b) cha katiba ya kenya kinasema
rais anafaa kuapishwa siku ya saba inayofuata
siku ya kutolewa kwa uamuzi wa mahakama wa kuidhinisha uchaguzi iwapo
kukiwa na kesi iliyokuwa imewasilishwa.
Hata hivyo kwa mujibu wa katiba rais anafaa kuapishwa
hadharani mbele ya jaji mkuu au naibu jaji mkuu.
No comments