TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI ZA AFRIKA ZINAZOKUWA KIUCHUMI
Mkurugenzi wa uchumi wa benki kuu ya
Tanzania bwana Johnson Nyella amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za afrika
zenye viwango vya juu vya ukuaji wa
uchumi katika kipindi cha muongo mmoja
uliopita 2016/2017.
Amesema uchumi wa tanzania ulikuwa
kwa wastani wa asilimia 6.7 mwaka 2016 wakati pato la taifa
lilikuwa kwa wastani wa asilimia 7 sawa
na ilivyo kuwa mwaka 2015 na 2014.
Ameyasema hayo wakati wa sherehe za siku ya
takwimu amabazo zilifanyika kitaifa jijini dar es salaam nakufafanua
kuwa mfuko wa bei wa taifa umeendelea kupungua na kubaki katika kiwango cha
tarakimu moja.
No comments