TANZANIA YAPEWA MKOPO WA MASHARTI NAFUU NA BENKI YA DUNIA
Benki ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 150 sawa na shilingi bilioni 340 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa kufungua fursa za utalii katika ukanda wa kusini mwa Tanzania
Akisaini mkataba wa mkopo huo katibu mkuu wa wizara ya fedha na mipango bw.Doto James amesema mkopo huo unalenga kuimarisha miundombinu ya utalii katika ukanda huo ikiwemo ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege,madaraja pamoja na kuibua fursa mbalimbali za utalii kuvutia watalii wengi zaidi
Mwakilishi mkazi wa benki ya dunia hapa nchini bi Bella Bird amesema kuwa mkopo huo ulioridhiwa na bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo jijini Worshington DC septemba mwaka huu umelenga kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta ya utalii na kupunguza umaskini kwa wananchi.
No comments