Heade

WAFANYAKAZI MIZIGO HAWATAVUMILIWA

Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa mh Seleman Jafo amesema hatavumiliana kuwa na wafanyakazi  mizigo ambao hawatimizi majukumu yao kikamilifu na keleta mabadiliko katika sekta ya barabara ambayo ni nguzo ya uchumi nchini.
ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wabunge wa kamati ya kudumu serikali zaa mitaa  TAMISEMI Sambamba na kamati ya hesabu za serikali za mitaa LAAC ambayo inafanyika katika ukumbi wa hazina mjini dodoma.
aidha mh Jafo ameeleza kuwa serikali  imeisha toa mwongozo wa malengo ya utendaji kazi katika utumishi wa umma na kuwa pima kulingana na malengo yao hivyo watumishi ambao watashindwa kutekeleza na kufikia malengo waliyo pangiwa na serikali haitasita kuwachukulia hatua za kiutumishi.


No comments

Powered by Blogger.