WALIOHAMISHA FADHA ZA SERIKALI WATAKIWA KURUDISHA
Rais mpya wa
Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza msamaha wa miezi 3 kwa watu binafsi na
kambuni mbalimbali kuzisalimisha fedha
za umma ambazo zimefichwa kinyume cha sheria nje ya nchi hiyo.
Amesema waliohusika wanatakiwa kutumia fursa ya miezi
3 kurejesha fedha hizo na mali walizoficha kinyume na sheria ili kuepukana na
aibu na kukubwa na mkono wa sheria.
Ameongeza kwamba
serikali itawakamata na kuwafungulia mashtaka wale watakaokataa kutii agizo
baada ya msamaha huo kumalizika ikiwa ni moja ya ahadi yake ya kupambana na
rushwa.
No comments