WAZIRI MKUU WA LEBANON AYAPA UHAKIKA MABENKI
Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri amewahakikishia wadau wa mabenki katika
eneo la Mashariki ya Kati hii leo kuwa suala la uthabiti wa Lebanon ndilo lenye
umuhimu mkubwa kwa upande wake. Matamshi hayo ya Hariri yanakuja ikiwa ni siku
moja tangu arejee nchini humo na kusitisha tangazo lake la kujiuzulu alilolitoa
wakati akiwa nchini Saudi Arabia na kusababisha mkwamo wa kisiasa nchini humo.
Akizungumza katika kongamano la
mabenki la nchi za Kiarabu mjini Beirut, Hariri amesema serikali yake itatoa
kipaumbele kwa masuala yenye masilahi na nchi hiyo zaidi kulinganisha na
changamoto zinazokabili ukanda huo.
Aidha Kundi la wabunge wa chama cha
Hezbollah nchini Lebanon katika taarifa yake limesema hii leo kuwa kurejea kwa
Saad Hariri na kauli yake ya matumaini kunaashiria hali kurejea kuwa ya kawaida
nchini humo.
No comments