WIKI iliyopita Korea Kaskazini ilifanya jaribio la kombora la masafa
marefu ambalo ilisema kuwa linaweza kufika popote nchini Marekani.
Kombora hilo mbali na kuzidisha uhasama na jirani zake pamoja na
Marekani, pia lilizua tafrani kwa abiria waliokuwa katika ndege eneo la
anga la Japan. Wahudumu wa ndege ya Shirika la Cathay Pacific iliyokuwa
katika anga ya Japan waliripoti kuona Kombora la Korea Kaskazini
lililokuwa likifanyiwa majaribio nchini humo.
Shirika hilo lilithibitishia BBC kuwa wahudumu wa ndege waliona kitu
ambacho kilikisiwa kuwa kombora hilo likiingia kwenye anga ya dunia.
Korea Kaskazini mara nyingi haitangazi pindi inapotaka kufanya majaribio
ya makombora yake na wala haitoi tahadhari na hata njia mbayo hupitia
mara nyingi haijulikani.
Hiyo ni kutokana na nchi hiyo kutokuwa na uwezo wa kupata data ya
safari za angani ili ipate kuelewa kabla ya kufanya jaribio lolote la
kombora. Kombora hilo lililotajwa kuwa lenye nguvu zaidi lilianguka
katika maji ya Japan lakini japokuwa ndilo kombora lililopaa mbali zaidi
kuliko kombora lolote lililofanyiwa majaribio na taifa hilo la
Kikomunisti.
Jaribio hilo lilizua msukosuko zaidi kati ya Korea Kaskazini na
majirani zake pamoja na Marekani, ambao Jumatatu walianzisha mazoezi yao
makubwa zaidi ya angani kuwahi kufanywa, ambayo yametajwa na Korea
Kaskazini kuwa uchokozi.
No comments