KAMANDA
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amewataka
askari kufanya mazoezi ya viungo ili kujiweka imara sambamba na kujenga
afya zao.
Kamanda Mambosasa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati
aliposhiriki katika matembezi na mazoezi ya viungo na askari wa vikosi
vya Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Alisema askari na jamii kwa ujumla
wanapaswa kufanya mazoezi pale wanapopata nafasi na siyo mpaka
walazimishwe, kwani mazoezi yanasaidia kujenga mwili na kuepusha mwili
na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu.
“Mazoezi haya yanatakiwa kuwa endelevu kwa askari wote wa polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, mazoezi haya yanajenga urafiki na
kuimarisha ujirani mwema na pia yanaweka mwili imara,” alisema.
Matembezi hayo ya ‘Root Match’ yalifanyika katika mikoa ya kipolisi
Temeke na Kinondoni na yatakuwa yakifanyika kila Jumamosi ya mwisho wa
mwezi
No comments