MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amezindua rasmi sheria
ndogondogo za uhifadhi rasilimali na utunzaji mazingira ya vijiji vyote
vilivyoko katika halmashauri ya wilaya ya Igunga na Mamlaka ya mji huo
na kuonya kuwa atakayekamatwa akiharibu na kuchafua mazingira atafi
kishwa mahakamani.
Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Makomero na Mwabakima vilivyoko
wilayani humo katika hafla ya uzinduzi wa sheria hizo, alisema
mazingira ya wilaya hiyo sasa yatakuwa bora kwa kuwa vitendo vya
uharibifu vitadhibitiwa.
Alisema kukithiri kwa vitendo vya ukataji miti ovyo, kuchoma moto,
kuharibu vyanzo vya maji na kujisaidia ovyo kulichangiwa kwa kiasi
kikubwa na ukosefu wa sheria zinazoweza kuwabana wahusika katika vijiji
na mamlaka ya mji.
Mwanri alifafanua kwa kuwa sheria hizo zimependekezwa na wananchi
wenyewe, hata zilipofika ofisini kwake hakusita, alizipitia na kusaini
moja kwa moja, hivyo akawataka kuzitekeleza ipasavyo ili kujiletea
maendeleo.
Aliwataka wenyeviti wa vijiji, watendaji na madiwani kuzisambaza na
kuhamasisha wananchi wao kuzisoma na kuzielewa ili watambue hatua za
kisheria zitakazowakabili punde watakapokwenda kinyume nazo.
Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji, Mwenyekiti wa serikali ya kijiji
cha Makomero, Zefania Kilo alimpongeza Mkuu wa Mkoa kwa kuzindua sheria
hizo na kwa kuanzia alisema atahakikisha kila kaya inakuwa na choo bora
na kupanda miti isiyopungua mitano.
No comments