WA N A N C H I wanaoishi karibu na nguzo za umeme hapa nchini,
wametakiwa kulinda kwa nguvu zao zote kwa kushirikiana na serikali za
vijiji ambazo nguzo hizo zimepita kwani kwa kufanya hivyo kutasaidai
kupunguza hujuma zinazoweza kujitokeza.
Meneja wa njia kuu za umeme nchini, Amos Kaihura alisema hayo wakati
akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mgongoro na Makomero, wilayani
Igunga baada ya kutokea tatizo la kufunguliwa kwa njia ya umeme ya
msongo mkubwa wa kilovati 400.
Alisema wananchi ndiyo wana jukumu ya kulinda miundombinu hiyo kwa
sababu wao ndiyo wapo kwenye maeneo ambayo nguzo hizo zinapita na
kuongeza kuwa hujuma hizo zimekuwa zikifanyika maeneo yao lakini
wamekuwa hawatoi taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya
kuwadhibiti watu wanaofanya uhalifu huo.
Kaihura alisema kutokana na kufungua nguzo hizo, tatizo kubwa
lingeweza kujitokeza nchini kwa wananchi wa mikoa ya Iringa, Dodoma,
Singida, Tabora na mikoa ya Kanda ya Ziwa ingeweza kukosa umeme na
kulisababishia taifa hasara kubwa.
Meneja huyo alisema serikali imewekeza kwa ajili ya wananchi kupata
umeme wa uhakika lakini wahuni wachache wanataka kuharibu miundombinu ya
umeme huo uliopo katika gridi ya taifa kutoka mkoani Iringa kwenda
Kanda ya Ziwa
No comments