Miji
mbalimbali ya California nchini Marekani imeendelea kukumbwa na visa
vya moto wa nyika. Tayari serikali ya jimbo hilo imeagiza shughuli mpya
ya kuhamisha watu baada ya moto mkubwa kushindwa kudhibitiwa siku ya
Jumapili kusini mwa jimbo la California.
Agizo
la kuhama limetolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu sehemu za
Carpinteria karibu na msitu wa Los Padres kilomita 160 kutoka Los
Angeles.
Vyanzo kadha vya Zima Moto vinasema moto huo wa nyika wa
Thomas, unatishia mji wa pwani wa Santa Barbara na mwingine ulio karibu
wa Carpinteria.
Awali wazima moto walisema kuwa moto huo ulikuwa
unadhibitiwa lakini walishindwa kutokana na ukubwa wa moto huo na
kuteketeza eneo lenye ukubwa wa jimbo la Chicago.
Hata hivyo
wazima moto hao wanasema moto mwingine katika jimbo hilo umedhibitiwa
kwa sehemu kubwa, lakini moto wa Thomas bado unaendelea kuteketez
amisitu na umedhibitiwa kwa asilimia 15 tu.
Siku ya Jumamosi
Gavana wa California Jerry Brown aliitaja hali hiyo kuwa mpya na kusema
kuwa moto huo unaochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa utatokea kila
mwaka.
Wadadisi wanasema huenda moto huo ukaharibu sekta ya thamani ya mamilioni ya dola ya kilimo katika jimbo la Carlifonia.
Watu
200,000 wamehamishwa kutoka makazi yao katika jimbo hilo na kuharibu
nyumba 800, huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki na wazima moto kadhaa
wamejeruhiwa kufuatia moto huu wa sasa unaoendelea.
No comments