Tume
ya Uchaguzi nchini Liberia (NEC) imetangaza kwamba duru ya pili ya
uchaguzi wa urais nchini humo itafanyika Desemba 26 kati nyota wa zamani
wa mpira wa miguu George Weah na Makamu wa Rais, Joseph Boakai,
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jerome Korkoya, ametangaza.
"Kulingana
na maagizo ya Mahakama Kuu kwa Tume ya Uchaguzi (...) duru ya pili ya
uchaguzi wa urais 2017 itafanyika Jumanne, Desemba 26," Bw Korkoya
alisema katika mkutano na waandishi wa habari, huku akiongeza kuwa
kampeni ya uchaguzi tayari imefunguliwa hadi Desemba 24 saa 05:59 usiku.
Duru
ya pili, ambayo awali iliyopangwa kufanyika Novemba 7, iliahirishwa na
Mahakama Kuu, ambayo iliamuru NEC kuchunguza madai ya mgombea, ambaye
alichukua nafasi ya tatu katika duru ya kwanza Oktoba 10, akipata 9.6%
ya kura, Charles Brumskine, ambaye Bw Boakai alijiunga naye.
Lakini
Mahakama ilifutilia mbali madai hayo, kwa kura nne dhidi ya moja, na
hivyo kuruhusu duru ya pili ya uchaguzi kufanyika, kwa masharti kwamba
NEC irejelee upya orodha za uchaguzi, zilizokosolewa, kwa mujibu wa VOA Afrique.
"Tunafahamu
kwamba siku hii ni baada ya Krismasi, na tunatoa wito kwa wapiga kura
wote waliosajiliwa kuchangia ili kufanikisha hili, kwa mapenzi ya
demokrasia yetu," Bw Korkoya aliongeza.
No comments