Haya ni majina ya wanajeshi 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania
(JWTZ), waliouawa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
wakati wakilinda amani.
Wanajeshi hayo ni Hamad Haji Bakari, Chazil Khatibu Nandonde, Idd
Abdallah Ally, Juma Mossi Ally, Ally Haji Ussi, Pascal Singo, Samwel
Chenga, Deogratius Kamili, Mwichumu Vuai Mohamed, Hassan Makame, Issa
Mussa Juma, Hamad Mzee Kamna, Salehe Mahembano na Nazoro Haji Bakari.
Tayari miili ya marehemu hao imeshaagwa katika viwanja vya ulinzi
vilivyopo makao ya jeshi yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wa Serikali wengine waliongoza
Watanzania kutoa heshima za mwisho kwa askari hao.
Askari hao 14 walifariki dunia katika mapigano na waasi wa kikundi cha
ADF nchini DRC, huku 44 wakijeruhiwa na mmoja akipotea baada ya kambi
yao kuvamiwa eneo la Mashariki mwa nchi Desemba 7 wakati wakitekeleza
majukumu ya ulinzi wa amani.
No comments