Heade

HATIMAYE NGUZA VIKING NA PAPII KOCHA WAACHIWA HURU

IKIWA ni siku ya Jumamosi tarehe 9 Desemba, 2017 katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma ambako maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara yamefanyika, ndipo Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama alitoa tangazo lililowasisimua watanzania wakashindwa kujizuia na kushangilia kwa nguvu zote.

Tangazo hilo sio lingine ni la kuwaachia huru wanamuziki mashuhuri kutoka DRC waliokuwa wamefungwa maisha katika magereza hapa nchini, Nguza Viking maarufu kama ‘Babu Seya’ na mwanawe Papii Kocha ambao ni wanamuziki wa muziki wa dansi wanaopendwa zaidi Tanzania.

Kwa muda mrefu watanzania wamekuwa na hamu ya kuwaona wanamuziki hao wakiwa huru waendelee na sanaa yao ya muziki lakini siku zote ndoto zao hizo hazikuwahi kutimia.

Lakini leo Rais Magufuli amekata kiu ya watanzania wengi kwa kuwaachia huru wanafamilia hao. Miaka 13 imepita tangu familia hiyo walipohukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 kwa kosa la kubaka.

Majaribio kadhaa ya rufaa zilizokatwa na wanasheria nguli hapa nchini yaligonga mwamba kwa nyakati tofauti lakini leo huruma ya Rais Magufuli hatimaye imewatoa.












































No comments

Powered by Blogger.