Heade

TATIZO LAKO SI KITU MBELE ZA BWANA MWAMINI YESU




Matatizo yapo duniani na hakuna mwanadamu anayependa kuishi huku akikabiliwa na matatizo, yapo matatizo mengi     yanayowasumbua watu katika nyanja mbalimbali,matharani wapo wanaosumbuliwa na hali ngumu ya kiuchumi,Mahusiano na Afya.
Kuna matatizo yanayosababishwa na mtu mwenyewe kwa kukosea baadhi ya mambo katika mazingira yanayomzunguka na mengine husababishwa na mwasisi wa matatizo katika ulimwengu huu.
Ibilisi aliasisi matatizo tangu pale alipovuruga mambo kule Edeni kwa kupitia wazazi wetu wa kwanza ADAM na HAWA.
Sina nia ya kukupeleka huko sana lakini napenda kukumbusha kuwa matatizo unayo yaona yakiwasumbua watu, kama hayakusababishwa na mtu mwenyewe basi ibilisi ndiye mwasisi wa matatizo hayo.
Baada ya kuwa umekubaliana na mimi, nikwambie kuwa kuna njia pekee ya kuyashinda ama kuondokana na tatizo linalokusumbua pasipo kutumia gharama kubwa kama unavyofikiri.
Njia pekee ya kulishinda tatizo linalokusumbua ni kukubali na kuamini  kupata msaada kwa yule mwenye uwezo wa kuyafutilia mbali matatizo yaliyoasisiwa na ibilisi.
Ukisoma Biblia takatifu kitabu cha Marko 9: 14-27 Utaona habari za kijana aliyeteswa na pepo bubu na kila alipompagaa alianguka chini, akitokwa na povu na kusaga meno na mara nyingi alimtupa katika moto na katika maji ili amwangamize.
Na mzazi wa kijana huyu anamwambia YESU  kuwa tatizo hili lilimpata kijana huyu toka utoto wake.

No comments

Powered by Blogger.