Kesi ya kumjeruhi mpaka kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho inayomkabili
mwalimu wa sanaa ya kujihami, ‘Martial Arts’ na msanii wa filamu za
kibongo, Salum Njwete maarufu Scorpion hatimaye imefikia tamati ambapo
hukumu inatarajiwa kusomwa januari 10 mwakani.
Kesi hiyo iliendelea jana katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya
Ilala jijini Dar ambapo Scorpion alikuwa akibanwa maswali na wakili wa
utetezi, Nassoro Katuga kufuatia utetezi wake alioutoa kipindi
kilichopita akiongozwa na wakili wake, Juma Nassoro.
Katika utetezi wake wa awali Scorpion alisema alishurutishwa kutoa
maelezo katika kituo cha polisi cha Buguruni ambapo wakili Katuga
alimuuliza kwanini alisaini.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Flora Haule aliifunga kwa kuahidi
kuitolea hukumu Januari 10 mwakani ambapo kabla ya hukumu hiyo kesi hiyo
itatajwa tena mahakamani hapo Desemba 27 mwaka huu.
No comments