Umoja
wa Ulaya umeionya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo kuwa
utasitisha misaada yake kusaidia nchi hiyo kufanikisha Uchaguzi Mkuu
mwaka ujao, iwapo itaendelea kutumia maafisa wa usalama kuwanyanyansa
wanasiasa wa upinzani na mashirika ya kiraia.
Katika
ripoti yake Umoja wa Ulaya umesema serikali ya Kinshasa imeendelea
kuwakamata, kuwazuia wanasiasa wa upinzani na wafuasi wao pamoja na
wanaharakati wa haki za binadamu kwa sababu ya harakati zao za kuikosoa
serikali ya rais Joseph Kabila.
Upinzani umefurahishwa na ripoti
hiyo. Akihojiwa na RFI, Gregoire Kiro, mbunge wa chama cha upinzani cha
RCD-Kml akiwa Kinshasa amesma hatua hiyo itapelekea visa vya unyanyasaji
vinavyoendelea kusitishwa mara moja.
Upande wa serikali, wao
wanaona kuwa Umoja wa Ulaya hauna sababu ya kutoa mashinikizo yoyote
wakati mchakato wa uchaguzi unaendelea vizuri.
Mbali na Umoja wa
Ulaya, Ubelgiji ambao ni wakoloni wa zamani wa DRC, wamesema wametenga
Euro milioni 5.8 kuisaidia Tume ya Uchaguzi kufanyika hilo.
Tume ya Uchaguzi nchini DRC CENI tayari imetangaza kuwa Uchaguzi Mkuu utafanyika mwezi Desemba mwaka ujao.
No comments