Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko tayari
kwa mazungumzo na viongozi wa kisiasa nchini humo kwa lengo la
kuendeleza maendeleo ya nchi hiyo.
Rais
Kenyatta ametoa kauli hii, wakati akiwahotubia raia wa nchi hiyo katika
maadhimisho ya miaka 54 ya uhuru, yaliyofanayika jijini Nairobi.
Kiongozi
wa upinzani NASA, Raila Odinga ambaye kuapishwa kwake kama rais wa
wananchi, kuliahirishwa leo, amekuwa akisema kuwa yuko tayari kwa
mazungumzo ambayo yatalenga kuwepo kwa Uchaguzi mpya wa urais, lakini
Kenyatta amesema hawezi kushiriki katika mazungumzo hayo kwa sababu
msimu wa kisiasa umepita.
Raila Odinga ambaye anaendelea kupinga
kuchaguliwa kwa rais Kenyatta na Stephen Kalonzo Musyoka, walikua
wanatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne Desemba 12 kama rais na makamu wa
rais mtawalia wa Jamhuri ya Kenya. Lakini Jana Jumatatu muungano huo
ulijirudi na kusema shughuli ya kumuapisha kiongozi wao imeahirishwa kwa
tarehe nyingine ambayo haikutajwa.
Wajumbe kutoka nchi za
magharibi na Kanisa wanapendelea mazungumzo kati ya rais Kenyatta na
Odinga yafanyike kufuatia wasiwasi kuwa njia iliyochaguliwa na upinzani
ilikuwa inalenga kuzusha machafuko.
Siku ya Jumamosi rais Kenyatta alisema hayuko tayari kwa mazungumzo yoyote kuhusu mabadiliko ya uchaguzi.
Shinikizo
zimekua zikiongezeka kumtaka kiongozi wa muungano wa upinzani nchini
Kenya kuachana na mpango wake wa kuapishwa kama rais wa watu siku ya
Jumanne Desemba 12.
Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifanyika tarehe 26 mwezi Oktoba ambapo Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.
Uchaguzi
huo wa tarehe 26 ulikuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama
ya juu nchini nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 mwaka
2017.
No comments