Madaktari wafutwa kwa kutangaza kimakosa kuwa mtoto alikufa India
Hospitali kwenye mji mkuu wa India, Delhi imewafuta kazi madaktari
wawili waliotangaza kimakosa kuwa mtoto aliyekuwa amezaliwa alikuw
amekufa.
Madaktari kwenye hospitali ya kibinafsi ya Max, walikuwa wametangaza
kuwa mtoto alikuwa amekufa saa kadhaa baada ya pacha wake kuzaliwa akiwa
amekufa tarehe 30 Novemba.
Wazazi waligundua kuwa mtoto huyo alikuwa hai wakati wakiwa njiani kwenda kumzika.
Kisa hicho kilizua ghadabu na mjadala kuhusu huduma za hospitali ya kibinafsi ambazo mara nyingi ni ghali mno,
Kisa hicho kilitokea wakati wazazi waligundua kuwa mmoja wa watoto hao
alikwa hai ndnai ya mfuko wa plastiki ambao madaktari walikuwa
wamemweka.
Kulingana na babu yake mtoto huyo, familia hiyo iliyokuwa imepigwa na
mshango na kumkimbiza mtoto huyo hospitalini ambapo waliambiwa kuwa
mtoto wao bado alikuwa hai.
No comments