Mkutano wa chama tawala nchi Zimbabwe cha Zanu-PF
unafanyika wiki hii nchini humo kuanzia leo Jumanne, Desemba 12 hadi
siku ya Ijumaa. Utakua mkutano mkuu wa kwanza wa chama hiki bila kuepo
kwa rais wa zamani Robert Mugabe.
Katika tukio hili, rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, anatarajia kuteua makamu wake wawili.
Mkutano
huu ulikua fursa kwa Robert Mugabe kumfuta kazi makamu wake Emmerson
Mnangagwa. Lakini hali hiyo ilibadilikakabla ya mkutano huo.
Chini
ya mwezi baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyosababisha kujiuzulu kwa
Robert Mugabe, Emmerson Mnangagwa anapaswa kuthibitishwa kama kiongozi
mkuu wa chama. Na kuteuliwa kama mgombea wa Zanu-PF katika uchaguzi ujao
uliopangwa kufanyika kabla ya mwezi Agosti 2018.
Hatua ya
kufukuzwa kwa Grace Mugabe, mkewe rais wa zamani Robert Mugabe, pia
ithibitishwa, pamoja na washirika wake wa karibu kutoka G40, Jonathan
Moyo, Saviour Kasukuwere na Makamu wa zamani wa rais Phelekezela Mphoko.
Lakini
taadsisi mbalimbali za chama cha Zanu-PF zitarekebishwa. Maveterani au
wapiganaji wa vita vya uhuru, waliotengwa kwa miaka kadhaa na Grace
Mugabe, wanatazamiwa kuchukua udhibiti wa nafasi muhimu.
Katika
tukio hili, rais Emmerson Mnangagwa atawateua Wajumbe Makamu wake
wawili. Mmoja kati kati ya watu hao ni Jenerali Constantino Chiwenga,
mkuu wa majeshi, alieendesha mapinduzi yaliyosababisha Robert Mugabe
kuachia ngazi.
Wiki iliyopita, serikali mpya iliwasilisha rasimu
ya bajeti ya mwaka 2018. Bajeti ambayo inaelekea kupata fedha za kigeni
ili kuvutia wawekezaji wa kigeni ambao waliikimbia nchi hiyo chini ya
utawala wa Robert Mugabe.
Kwa mujibu wa Philippe Van Damme, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Zimbabwe, hatua hizi ni nzuri, lakini hazitoshi.
No comments