Wanawake watatu wamejitokeza na kumtuhumu rais
Donald Trump kwamba aliwafanyia ukatili wa kijinisa bila ridhaa yao
miaka iliyopita,
huku wakiombabunge la wawakilishi kumchunguza kutokana
na kashfa hizo.
Jessica Leeds,
Samantha Holvey, na Rachel Crooks wamesema kuwa rais Trump alikuwa
akiwabusu kwa nguvu akiwashika shika na kuwafanyia ukatili mwingine.
Hata hivyo msemaji wa ikulu ya White House, Sarah Huckabee Sanders, amesema kuwa madai hayo hayana msingi wowote na ni uzushi.
Baadhi ya wanawake hao wamedai kuwa walilazimishwa kufanyiwa ukatili huo kama vile kupigwa busu na ukatili mwingine.
Samantha
Holvey amesema, Trump alikuwa akiwakagua mwilini wakati alipokua
akihudhuria mashindano ya Wasichana Warembo mwaka 2006. Lakini amesema
hana nia ya “kumchukulia hatua bali anaweka wazi dhulma aliofanyiwa.
Rais
Trump tangu achukue hatamu ya uongozi wa Marekani amekua akikabiliwa na
tuhuma kama hizi ikiwa ni pamoja na kashfa za ukwepaji kodi na zile za
kisiasa.
No comments