MWALIMU wa Shule ya msingi, Itiryo tarafa ya Ingwe wilayani Tarime
mkoani Mara, Samwel Mariba Daniel (29) amefikishwa katika mahakama ya
wilaya Tarime akituhumiwa kuwabaka wanafunzi wake tisa wenye umri wa
chini ya miaka 10 kwa nyakati tofauti kuanzia mwezi Agosti na Novemba
mwaka huu.
Akisomewa mashitaka hayo ya ubakaji katika kesi ya jinai namba
682/2017 mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Amon Kahimba,
Mwendesha Mashitaka wa Polisi Inspekta Saumu Ngoma alidai kuwa mtuhumiwa
Mariba alitenda makosa hayo kati ya ubakaji kwa nyakati tofauti kwa
wanafunzi wake wa darasa la kwanza na la pili kati ya Agosti na Novemba
mwaka huu 2017.
Mwendesha mashitaka alidai kuwa, wanafunzi hao wa kike chini ya miaka
10 ambao majina yamehifadhiwa walibakwa na mwalimu huyo kwa nyakati
tofauti wakati wakiwa maeneo ya shule hiyo kwenye nyumba za walimu.
Alidai mwalimu alikuwa akiwatuma na kisha wanapokuwa ndani ya nyumba
alikuwa akitenda kosa hilo
No comments