Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo
amekamatwa na serikali baada ya kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali .
Mwanasheria huyo amekamatwa kwa amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo
ambapo pamoja na mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha
shughuli zake bila kufuata sheria ya mazingira .
Akiwa katika katika ziara ya kikazi ya siku mbili Wilayani
Geita,Mhe.Kangi Lugola ameagiza kukamatwa kwa mwanasheria huyo baada ya
kudaiwa kukutwa na nyaraka za serikali ambazo hazijawa rasmi kutumika
kutoka taasisi ya wakala wa utafiti wa jiolojia Tanzania(GST).
Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida na bila kutarajiwa.Mwanasheria
huyo aliyekuwa akiukingia kifua mgodi huo ili usikumbane na rungu la
fidia ya uharibifu wa kimazingira kama sheria inavyotamka, alijikuta
akimweleza Naibu Waziri kuwa anayo ripoti ya GST aliyodai haijaeleza
iwapo mgodi huo unahusika moja kwa moja kwenye uharibifu hivyo mgodi huo
usibebeshwe mzigo huo.
Kutokana na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe ripoti hiyo
ili ajiridhishe,lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka
kiongozi huyo wa juu kutumia mbinu zake kuipata Serikalini, lakini yeye
hawezi kutoa nyaraka ya serikali, jambo lililomkasirisha Naibu Waziri wa
Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.
Diwani wa kata ya mtakuja Constatine Morandi ameelezea kuwa wananchi
wamekuwa wakisumbuliwa muda mrefu na mgodi bila ya kupatiwa fidia na
kwamba kutokana na wao kuwa ndani ya bikoni kumesababisha kutokupatiwa
huduma mbali mbali za kijamii hivyo ni vyema kwa serikali wakaweka nguvu
kuwasaidia wananchi hao.
Bw Abdallah Omary-Mkazi Nyamalembo alimweleza Naibu waziri kwamba
wamekuwa wakiishi maisha ya mashaka kutokana na hali ilivyo ya maeneo
hayo ya mgodini na kwamba mgodi ulikwisha wai kuwapatia fidia ya
shilingi elfu ishirini jambo ambalo limeonekana kuwa ni udhalilishaji
kwani pesa hiyo ni ndogo.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa mgodi huo Saimon Shayo,alisema kuwa
eneo ambalo wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu suala la fidia hadi
sasa kuna nyumba mbili na kwamba fidia ya kwanza walilipa kiasi cha
sh,Bilion Moja na waliipatia serikali iweze kuwafidia wananchi
No comments