Serikali ya Zimbabwe kupitia Waziri wake mpya wa
kilimo, imeamuru kurudishwa kwa mashamba yaliyokua yakimilikiwa na
wakulima Wazungu, ambao walinyang'anywa wakati wa utawala wa Mugabe na
kupewa raia wa Zimbabwe.
"Wote
ambao wamewekwa kinyume cha sheria katika mashamba ambayo si mali yao
wanapaswa kuyarudisha haraka iwezekanavyo," alisema Perence Shiri,
Waziri mpya wa Kilimo wa Zimbabwe siku ya Alhamisi.
Waziri Shiri
alisema kuwa wale ambao wana vibali rasmi wataruhusiwa kuendelea kulima
katika mashamba hayo ili kuhakikisha uzalishaji.
Shiri alisema kuwa hatua hiyo inalenga kukuza kilimo kwa ajili ya uchumi wa nchi hiyo ambao unaendelea kudorora kila kukicha.
"Ikiwa
tunataka kufanikisha malengo yaliyowekwa na serikali na kutumia kilimo
kama nguzo ya uchumi, lazima tuhakikishe urasibu mzuri wa kilimo,"
waziri Shiri aliongeza.
No comments