MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya jiji la Tanga, Daudi Mayeji
amesema ufanisi kazini wa watumishi wa idara mbalimbali umeongezeka
baada ya kuanza kutumia kwa karibu mfumo wa kutathmini utendajikazi wa
wazi (OPRAS) unaoweka bayana majukumu na malengo ikilinganishwa na
ilivyokuwa awali.
Ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji wa
halmashauri hiyo kuhusu Utumishi na Utawala Bora kwa Waziri wa Nchi
ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George
Mkuchika alipotembelea baadhi ya wanufaika wa utekelezaji wa miradi ya
TASAF III jijini Tanga.
Mafanikio hayo amesema yametokana na hatua ya wilaya kuwekwa wazi
majukumu ya kazi, malengo ya utendaji, watumishi wote kukubali kuongozwa
na maadili ya ufanyaji kazi wa pamoja, uwajibikaji kwa ngazi zote
pamoja na Utawala Bora.
No comments