MKUU wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ameitaka polisi mkoani humo
kuwakamata watu waliowatia mimba wanafunzi 20 ambao walishindwa kufanya
mitihani yao ya kumaliza darasa la saba mwaka huu.
Aliyasema hayo mjini Kibaha wakati wa kikao cha bodi ya uteuzi wa
wanafunzi waliofaulu na wanaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2018 na
kuongeza kuwa wanafunzi hao wa kike ndiyo walioshindwa kufanya mitihani
yao ya kumaliza darasa la saba kutokana na kupata ujauzito kwenye mkoa
huo.
"Naagiza polisi kuwakamata watu hao waliowatia mimba wanafunzi
wakashindwa kufanya mitihani yao ya kumaliza darasa la saba mwaka huu,"
alisema Ndikilo na kuongeza kuwa sheria ziko wazi kwa wanaowatia mimba
wanafunzi hivyo wahusika hao wakamatwe wafikishwe mahakamani kujibu
tuhuma hizo.
Alisema haiwezekani kuwakalia kimya wahusika kwani wamewaharibia
maisha watoto hao ambao ndoto zao zimeyeyuka kwa kukatishwa na watu
wasio na utu hivyo.
No comments