Heade

WANAOKWAMISHA KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

Watendaji wa kata na vijiji ambao watabainika kukwamisha suala zima la kesi za mimba na ndoa za utotoni watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Ofisa maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Chamwino, Sofia Swai alisema wilaya hiyo imeamua kuweka mikakati hiyo ili kuwabaini wanaokwamisha kuchukuliwa hatua kwa wale wanaobainika kuwapa mimba watoto wa shule. Alisema hayo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na viongozi wa kata za Mpyayungu, Mlowa Barabarani, Mlowa Bwawani, Manchari, Msanga na Chilonwa.
Alisema kuwa azimio hilo limekuja kufuatia mkuu wa wilaya hiyo kusema kuwa ili nidhamu iweze kujengeka ndani ya wilaya hiyo na matukio hayo ya mimba na ndoa za utotoni yaweze kuisha ni lazima wapatikane viongozi hata wawili wanaokwamisha na wachukuliwe hatua kali.
“Hivi sasa wilaya yetu inatafuta kitu ambacho kimejificha hapo katikati ambacho bado kinakwamisha suala hili lisiweze kwisha katika wilaya yetu na ndiyo maana tumeamua kuwapa mafunzo watendaji wa kata, watendaji wa vijiji, walimu, wanasiasa na viongozi wa dini ili waweze kujitambua katika nafasi zao na kutoa haki,”alisema Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo yanafanywa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Women Wake Up (WOWAP) kupitia ufadhili wa The Foundation For Civil Society katika mradi wa kupunguza ukatili na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Wowap, Nasra Suleiman alisema kuwa hivi mradi huo upo katika awamu ya nne na kazi kubwa wanayoifanya ni kuwapa mafunzo viongozi hao ili waweze kufanya kazi kama timu. Mwalimu Daniel Wami akizungumza mra baada ya kupata mafunzo hayo alisema anaona serikali itunge sheria ya mtu atakayempa mtoto wa shule mimba afungwe miaka 30 na binti aliyekubali kushawishiwa naye afungwe miaka 15 hiyo itakuwa fundisho.

No comments

Powered by Blogger.